Utangulizi
Kwetu afya,tuna malengo makubwa Zaid kukuelimisha wew mwananchi wa kawaida ili ujikwamue kiuchumi kupitia elimu zitolewazo nasi ""kwetu afya""
Nin tofauti ya tiba na kinga(chanjo)
Tiba,
Ni kitendo cha kutoa dawa kwa mnyama aloadhira na ugonjwa kwa dawa inayotibu ugonjwa huo
Kinga(chanjo)
Ni hile hali ya kuweka uimara kwa mnyama kabla ya ugonjwa haujatokea kwa kuwapa chanjo kwa kuzuia magonjwa husika
MAGONJWA YA KUKU:
Kuna aina nying ya magonjwa yanayo shambulia kuku baadhi yao ni kama haya:-
- Mdondo (Newcastle)
- Gumboro
- Ndui ya kuku
- Upungufu wa vitamin A
- Koksidiosis
- Minyoo ya michango
- Viroboto (utitiri)
MDONDO (Newcastle)
Huu ni ugonjwa unaosababishwa na virusi kwenye kuku
Dalili zake
- Kuku kuacha kula(ukosefu wa hamu ya kula)
- Kutoa machoz na makamasi puani
- Hupumua kwa shida
- Kuku kupooza
- Kuzungusha kichwa na kutembea kinyume nyume
- Ugonjwa huu hauna dawa Wala tiba
- Bali ugonjwa huu hutumia Kinga au chanjo kuwakinga kuku
- Chanjo yake itatolewa kila baada ya miezi mitatu kabla ya kuku kuugua
- Tumia Newcastle vaccine kuchanja kuku wako
Huu ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi
Virusi hizo husambazwa kwa kinyesi cha kuku aliyeadhirika
Kirusi hiki ni vigumu kukiondoa kwenye mazingira
Dalili zake
- Kuku huarisha majimaji
- Dalili zingne huanza kuoneka baada ya wiki sita au kumi na nane baada ya kuku kuugua
- Ugonjwa huu hauna dawa bali hukingwa kwa kuwachanja kuku kabla ya kuugua
- Safisha mazingira na Banda wanamo lala kuku
- Safisha vyombo wanavyotumia kukia chakula na maji
- Tumia gumboro vaccine kuchanja kuku wako
Ndui ni ugonjwa unaosababishwa na virusi na huathiri sana vifaranga,pia ugonjwa huu hujitokeza sana wakati wa mvua
Tiba na kinga
- Dawa za kuua vimelea Kama vile joto ya vidonda
- Chanjo ya sindano itolewe kabla ya msimu wa mvua kuanza
- Pia waweza kutumia dawa aina ya otc plip kupooza madonda
Huu Ni ugonjwa unaojitokeza baada ya kuku kukosa vyakula vyenye vitamin A kwa mda mrefu
Kuku wadogo ndo huadhitika sana na tatizo hili
Dalili zake
- Macho kuvimba na kutoa uchafu mzito Kama sabuni iloyoloana
- Kuku hudhoofika hatimaye kufa
- Wapatie kuku vyakula vyenye vitamin A kwa wingi
- Pia kinga ugonjwa huu kwa kuwapa kuku majani au michicha hasa wakati wa kiangazi
- Ugonjwa huu ukiingia hauna dawa
Huu ni ugonjwa wa vimelea huadhiri sana na kuua kuku wadogo kuanzia umri was wiku moja
Dalili zake
- Kiku hodhoofika
- Manyoya huvurugika na kuku kuzubaa
- Kuki kuvaa koti
- Huarisha kinyesi rangi cha damu au cha rangi ya kahawia
- Tumia dawa dawa aina ya aproliumu au sulfa
- Dawa hizi pia hutumik kuimarisha kinga kwa mda mrefu kwa kuku
- Hukaa timbon mwa kuku
- Dalili zake ni kama hz:-,hupunguza kutaga,kuku huarisha na pia kuku hupoteza uzito
Hivi ni vijidudu ambavyo hushambulia kuku kichwan na kunyonya damu.
Wadudu hawa huuwa sana vifaranga vidogo sana pia hivi hutokea sana wakati wa mvua nyingi au kuku wakiwa wanaatimia
Tiba na kinga
- Safisha mara kwa mara banda lsko hasa kuku wakisha totoa
- Tumia dawa za aina zote za dust zikiwemo,Akheri powder,ultravin dust,bakiller dust na sevin dust
Santen sana:imeandaliwa na dr john masiani na kutolewa kwenu na kwetu afya
Simu no:0756986228
Thanks for your cooperation