KILIMO CHA BAMIA






 BAMIA (OKRA/LADY FINGER)- (Abelmoschus esculentus)



1.UTANGULIZI


www.kwetuafya.blogspot.com

 Bamia ni zao lililo katika kundi ya mazao ya mbogamboga na likilimwa vizuri linaweza kumuongezea kipato mkulima wa zao hili pale atakapochuma na kuziuza.Bamia hutumika katika mapishi mbalimbali majumbani.Bamia hutumika kama kiungo cha machuzi au cha mboga au mboga kwa asilimia kubwa kanda za mwambao wa Pwani na Maeneo mengine.Bamia lina madini ya calcium kwa wingi.


2.HALI YA HEWA INAYOFAA KWA KILIMO CHA BAMIA

Bamia inaweza kulimwa katika ukanda wowote wa nchi ya Tanzania,Kutoka mita 0-1500 kutoka usawa wa bahari zaidi ya hapo unaweza kulima lakini halivumilii hali ya baridi kali..Lakini bamia hufanya vizuri zaidi katika maeneo yenye udongo wenye unyevu  wa kutosha na joto la wastani wa nyuzi joto 25 - 35 C.Pia maeneo ya ukanda wa chini yapatayo mvua hadi  kiasi cha milimita 1000 cha mvua kwa mwaka.


3.UDONGO UNAOFAA KWA KILIMO CHA BAMIA


Bamia hustawi vizuri katika udongo wenye rutuba ya kutosha  na zinaweza kulimwa katika udongo wa kichanga udongo mwepesi wa mfinyanzi.Bamia hustawi vizuri zaidi katika udongo ambao hautuamishi maji. Na udongo tifutifu ambao umeundwa na mchanga na mfinyazi  na ambao una kiasi kikubwa cha samadi hufaa zaidi kwa kilimo cha bamia.Zao hili hustawi zaidi katika udongo wenye p.H ya 6.0 hadi 7.


4.MAANDALIZI YA SHAMBA LA BAMIA


Shamba inabidi lisafishwe kwa kukata miti kama ipo kisha ling'olewe visiki,kama ni la kufyekwa nyasi lifyekwe kisha lilimwe kwa jembe la mkono au trekta au pawatilla au jembe la ng'ombe kisha udongo ulainishwe kuondoa mabonge mabonge yaliyopo. Kama utatawanya samadi kiasi cha tani 5-10 kwa ekari katika shamba lako kipindi cha kulima itasaidia kuboresha udongo www.kwetuafya.blogspot.com  wako na kuruhusu mzunguko mzuri wa hewa katika udongo wa shamba lako kwa ukuaji mzuri wa Bamia.kama utaweza andaa Matuta ambayo yataachana umabali wa sentimeta 60 kutoka tuta hadi tuta.

5.MBEGU BORA ZA BAMIA

Kuna aina mbalimbali za mbegu bora za bamia zinazoweza kupandwa na kutoa mavuno bora kama vile Lady’s Finger, Quim Bombo, Asutem, Mkulima-Clemson Spineless, Labadi Dwarf.


6.UPANDAJI WA BAMIA


Mbegu za bamia husumbua kidogo kuota kama zitakutana na hali ya kibaridi katika udongo.Hivyo ili ziote vizuri unashauriwa kabla ya kuzipanda shambani ziloweke katika maji ya uvuguvugu kwa masaa 24 au ziloweke kwa dakika 30 katika ethly alcohol and acetone,na uzipandae mbegu zako katika mashimo uliyoyachimba katika udongo wenye unyevu kwa kina cha sentimeta 2 -5 katika nafasi ya sentimeta 60-90 kati ya mstari na msatari na sentimeta 25-50 Kati ya shina na shina Kama kama hukutawanya mbolea ya samadi  wakati wa kulima utahitajika katika kila shimo uweke mbolea kwa ajili ya ukuaji mzuri wa Bamia zako Uanweza kutumia mbolea ya kuku au ng'ombe amabayo ni bora zaidi kwani ya kuku huisha kazi yake mapema zaidi katika udongo.Panda Mbegu mbili  kwa kila shimo na zikisha ota ngolea uache shina moja kwa kila shimo.kiasi cha kilo 1.5 - 2.5 hutosha kwa ekari moja ambapo wingi wa mbegu itategemea uwezo wa mbegu kuota na aina ya bamia.Kama mbegu zako uwezo wake wa kuota nia mdogo mbegu zitatumika nyingi na kama unapanda bamia fupi au bamia zenye mbegu kubwa  mbegu itatumika nyingi pia.Mbegu za bamia zinaweza kuchukua siku 8 - 10 kupandwa hadi kuota.Pia bamia unaweza kupanda mbegu katika kitalu baadaye zikifikisha sentimeta 10-15 unazing'oa na kwenda kupanda shambani ila njia nzuri ni kupanda moja kwa moja shambani. www.kwetuafya.blogspot.com


UMWAGILIAJI-Kama unyevu ni mdogo katika shamba lako itahitajika uwe unamwagilia shamba lako kila baada ya siku 10 au pungufu kulingana na hali ya unyevu katika shamba lako.Kiasi cha wastani wa milimita 350 za maji katika siku 10 zinahitajika kwa ukuaji wa bamia ili uweze kupata mavuno yaliyo bora na mengi.na kama umepanda mbegu katika kipindi cha ukame zimwagilie kila siku kuhakikisha udongo wako unakuwa na unyevu wa kutosha ili kuwezesha mbegu zako kuota. www.kwetuafya.blogspot.com

 


7.PALIZI NA KUPUNGUZA MIMEA YA BAMIA


Palilia mapema shmaba lako la bamia ilizikuwe vizuri zikiwa na afya bora,Baada ya wiki moja baada ya bamia kuota unaweza kuanza kuzipalilia kama shamba lako lina magugu.magugu yatagombea chakula na bamia hivyo kuzifanya zisikuwe vizuri.Unaweza kupalilia kwa Jembe la mkono au kwa kung'oa au jembe la aina yoyote ilimladi usiichubue mizizi www.kwetuafya.blogspot.com au shina la bamia.Wakati unafanya palizi ya kwanza pia utang'olea mashina/utapunguza mimea katika mashimo na kuacha mche mmoja kwa kila shimo.Pia uanaweza kurudishia kupandikiza miche uliyong'oa katika mashimo ambayo mbegu ziligoma kuota.


8.MBOLEA


Ili kuzifanya bamia zako ziwe na mavuno mazuri basi hakikisha kama shamba lako lina rutuba basi panda kwa kutumia mbolea ya samadi na Kama halina rutuba basi pandia mbolea ya samadi au N.P.K (15-15-15)/(10-15-15) kiasi cha kilogram 50 - 100 na au wakati wa Mibamia kuweka maua tumia mbolea ya Urea Kilogram 25-30 kwa ekari au SA kilogram 50 kwa ekari.


9.WADUDU NA MAGONJWA YA BAMIA


Bamia hushambuliwa na wadudu na magonjwa mbalimbali.


MAGONJWA YA BAMIA


Bamia hushambuliwa na magonjwa mbalimbali kama vile;

a) Ubwiri unga (Powdery mildew)

Ni ugonjwa unaosababishwa na fangasi(ukungu).ugonjwa ambao hufanya mmea kuwa na madoa au unga unga unga wa rangi ya kijivu katika majani na baadaye hunyauka na kufa na kupukutika majani.

TIBA NA KINGA

Liweke shamba lako katika hali ya usafi na Puliza dawa za ukungu zenye salfa kama vile copper sulphate, na siku za upuliziaji itategemea muda wa kulima bamia masika hupulizwa mara kwa mara na kiangazi hupulizwa mara chache.


 www.kwetuafya.blogspot.com

b)Ugonjwa wa kujikunja na kudumaa majani (Leaf curl)

ni ugonjwa unaosababishwa na virusi ni ugonjwa  ambao huambatana na kujikunja kwa majani machanga na kuwa magumu  na mmea kudumaa kukua.

KUZUIA NA KINGA-panda mbegu kinzani na ugonjwa huu,tumia madawa ya ukungu kama vile Copper sulphate, au puliza sulpha au copper  (BONIDE).Pia tumia dawa za wadudu kuua wadudu kama nzi weupe  ambao kwa kiasi kikubwa hueneza ugonjwa huu.


c) Ugonjwa wa manjano(Mosaic)

Ni ugonjwa unaosababishwa na virusi amabapo mmea ulioshambuliwa huwa na majani yenye umbo na ukubwa wa kawaida lakini yenye kijani kikavu au majani yenye rangi ya njano ambapo baadaye mmea hudumaa kukua.KUMBUKA rangi ya njano ya majani inaweza kusababishwa pia na ukosefu wa nitrojeni katika mmea hasa kama maji yatakuwa mengi ardhini katka udongo.

KUZIA NA KINGA

kukinga na kuzuia ugonjwa huu hakikisha unapanda mbegu kinzani na ugonjwa huu.zui wadudu katika shamba lako kwani wanaweza kueneza ugonjwa huu shambani kwako.Jiadhari na uvutaji au ubebaji wa  sigara/tumbaku katika shamba la bamia wakati unatembea au unafanya kazi katika shamba la bamia.Ng'oa mashina yaliyoathirika mapema na uyachome moto mbali na shamba.lima kilimo cha mzunguko wa mazao tofauti na jamii ya bamia.


 www.kwetuafya.blogspot.com


WADUDU WAHARIBIFU WA BAMIA


a)Mdudu mafuta (aphids)

Hufyonza majimaji katika majani na bamia changa hivyo kusababisha bamia kutokuwa vizuri na bora.

Kinga na tiba

Tumia dawa za wadudu kama vile ABAMECTIN,NIMEBECIDIN n.k

 


b)MIilibagi(Mealy bug)

Ni wadudu wanaoganda katika majani,matawi na bamia wakifyonza maji maji ya mimea.

Kuzuia na Kinga-Tumia dawa za wadudu kama vile selecron 720,Nimebecidin,multimectin n.kImage result for image of okra affected by mealybugs


c)Funza(Boll worm)

Hawa ni funza amabao hutoboa na kuharibu Bamia

Kinga na tiba

Kwa maeneo yanayoshambuliwa sana na wadudu,Puliza dawa za wadudu mara tuu bamia ziwekapo ua na zikiwa ndogo,Puliza asubuhi sana au jioni sana ili kuwakwepa wadudu wachavushaji wasije kufa na dawa wakati unapuliza.Puliza dawa kama vile Nimebedicin,albamectin n.k kuua wadudu hawa


d)Funga funga(Leaf roller)

hufunga majani kwa kuyavilingisha na kukaa na kula majani hayo.

kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin n.k


e)Inzi weupe (whitefly)

Ni waenezaji wakubwa wa magonjwa ya virusi, wadudu hawa hufyonza majimaji katika majani ya mimea na hujificha sana chini ya majani wakati wa jua kali.

kinga na tiba-zuia wadudu hawa kwa kuwaua kwa mikono au puliza dawa za wadudu kama vile nimebedicin,karate,multimectin n.k


f)Vinundu katika Mizizi(Root –knot nematodes)

Ni wadudu wadogo kama minyoo midogo ambao hula katika mizizi midogo na kusababisha uvimbe na mimea kusinyaa.

kinga na tiba

tumia dawa kama vile NIMEBECIDIN (kwa kiasi kikubwa Chini ya shina La mmea), DAZOMET (BASAMID),CARBOFURAN(FURADAN) kuua wadudu hawa.Hizi ni  dawa za ardhini.


10.UVUNAJI WA BAMIA

Bamia huwa tayari kuanza kuvunwa mwezi 1.5-2 tangu kupandwa na huckukua siku 3-6 kuvunwa baada ya ua kuanguka.kama matunzo ni mazuri kila ua katika mabamia litatowa bamia.chuma vizuri bamia kutoka katika mbamia bila kuacha athari kubwa katika mche wa mbamia.Hivyo kwa uvunaji mzuri unaweza kutumia mkasi mkali katika kukata vikonyo vya bamia.chuma bamia kubwa na ndogo ziache ziendelee kukua,ila inakubidi uwe mwangalifu ili bamia zisije kukomaa shambani kwani hukomaa kwa haraka zaidi na zilizokomaa hazina soko zuri na hazipendwi na walaji kwani huwa ngumu na nyuzinyuzi nyingi.Katika matunzo mazuri unaweza kuendelea kuchuma bamia kutoka katika mibamia kwa muda wa miezi miezi 2 na zaidi. www.kilimofaida.com

MAVUNO-wingi wa mavuno hutegemea matunzo na aina ya mbegu za bamia,muda wa upandaji na kukua-baridi ikiwa kali mavuno yake hupungua na mara za uchumaji wa bamia-kadri zinavyochumwa mara nyingi ndivyozinavyozidi kuzaa na zile zinazozachumwa kwa muda mrefu ndizo zenye manufaa kwa mkulima , japokuwa kwa wastani  bamia huvunwa kiasi cha tani 3 - 10 kwa ekari


Picha za uvunaji bora wa bamia

 Image result for image of okra harvesting


11.UHIFADHI WA BAMIA


Bamia kama yalivyo mazao mengine ya mbogamboga haistahimili kukaa muda mrefu bila kuliwa na kadri inavyokaa muda mrefu baada ya kuvunwa ndipo hupoteza ubora wake.Kama unasoko la uhakika hakikisha unazivuna na kuzipanga katika makundi kulingana na mahitaji ya soko lako.bamia zikishavunwa na kupangwa makundi au kama soko la kawaida ambalo halihitaji kuzipanga katika makundi ziweke katika boksi,tenga au ndoo na kuzisafirisha sehemu unayotaka kuzipeleka kuuza.Kwa wengine huzisindika na kuwawezesha kuzitunza na kuziuza kwa muda mrefu.

Post a Comment

Comment what you think about
© KWETU AFYA. All rights reserved. Developed by Jago Desain